TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI                                                                        31/01/2018

  • Wabunifu wa Tanzania wamazindua rasmi chama chao.
  • Chama cha Mitindo Tanzania kimezinduliwa tarehe 31 Januari 2017
  • Wabunifu wa mavazi Tanzania kuunga mkono sera ya “ Tanzania ya viwanda”

Wanamitindo wa Tanzania waungana pamoja katika kuanzisha chama chao, uzinduzi maalum wa Chama Cha Mitindo Tanzania umefanyika leo tarehe 31 Januari 2018 katika ukumbi wa habari maelezo jijini Dar es Salaam.

Chama cha Mitindo Tanzania (FAT) ni shirika lisilo tengeneza faida , lenye lengo la kundeleza maslahi ya sekta ya mitindo ya Tanzania kwa kuwaunganisha na kugawana ujuzi, uzoefu na rasilimali za sekta hiyo. Chama hiki kinatarajia kukuza sekta ya  mitindo ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau husika.

Mpango wa kuanzisha chama hiki ulitoka kwa Balaza la Sanaa Tanzania (BASATA) tupitia mkurugenzi wa Kukuza Sanaa na Masoko, Bi. Vivian Shalua, aliufikisha ujumbe huu katika uzinduzi wa maonyesho ya mavazi (SWAHILI FASHION WEEK 2017) uliofanyika tarehe 1 mwezi Novemba mwaka jana, alisisitiza kuwa wabunifu wa mavazi wa Tanzania wanapaswa kuanzisha chama chao ambacho kitatoa jitihada za ufanisi katika kupanga maamuzi na kushuhulikia mambo yote yanayohusisha wanachama wake, na kuwahamasisha kushiriki katika programu zinazofaidisha sekta nzima ya mitindo. Vile vile alimuhimiza mratibu wa maonyesho hayo aongoze katika kuhakikisha BASATA inatoa msaada wa kutosha katika kutimiza maslahi yao.

Akihutubia waandishi wa habari, Mwanzilishi wa Chama cha Mitindo Tanzania , Mustafa Hassanali alisema “ chama hiki (FAT) kimeanzishwa kuwa  chenye nguvu na  taaluma ya  uwezo wa kukuza na kuimarisha sekta ya mitindo nchini Tanzania. Sisi kama wabunifu tunaunga mkono juhudi za Raisi wetu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, katika kuifanya nchi yetu kuwa katika uchumi wa viwanda wa kati ifikapo mwaka 2025 kwa kuongoza katika bidhaa za nguo na vitambaa zinazotoka Tanzania”.

“Sekta ya mitindo Tanzania inakuwa kwa haraka sana, wadau wake wanakumbana na changamoto nyingi sana, lakini bado tuna uhakika wakati wa mafanikio umefika kupitia  kuanzishwa kwa chama hiki chenye nia ya kuimarisha uhusiano nzuri wa wafanyaji kazi za mitindo, wadau wa mitindo, na katika ngazi za serikali nchini Tanzania, Afrika na mataifa mengine” aliongezea mwanzilishi wa Chama cha Mitindo Tanzania (FAT).

Kwa mujibu wa Moja ya waanzilishi wa chama hicho, Bibi Asia Idarous, alisema  chama hicho hakijaundwa kwa ajili wa wabunifu tu, bali kwa wadau wote katika sekta ya mtindo, inajumuisha majukwaa mbalimbali ya mtindo, taasisi za mtindo, wanamitindo wa kuonyesha mavazi (models), wanamitindo wanopanga muonekano wa mavazi (stylist) , wapiga picha wa mtindo, Makampuni ya nguo, wazalishaji na wauzaji mavazi, na wengine wengi wanaoujiusisha na kazi za mitindo na urembo.

Aidha, aliongeza kuwa “nimetembea katika nchi nyingi duniani na kushiriki katika majukwaa mengi ya mitindo, lakini nchi zenye maendeleo makubwa katika sekta ya mitindo, ni zile zilifanya juhudi ya kuunda chama ambacho kitasimamia maslahi yao, bado hatujachelewa kufanya hivyo , changamoto zipo katika kila chama haswa chama kipya, ila tunajijengea utamaduni  na kutekeleza kazi za utawala ambazo zitaturuhusu sisi kufikia malengo yetu kama chama, nina hakika kwa sasa chama kimeanza vizuri”

Wafanyakazi katika sekta ya mitindo nchini wanahimizwa kujiunga katika chama hiki kwaajili ya kupaza sauti zao kwa fursa mpya za mitindo, kutatua changamoto za kazi za mitindo na kupanua mitandao yao katika nchi zote za afrika na zinginezo  ili kuongoza sera  ya “uchumi wa kati wa viwanda” kufikia 2025 ambayo inapiganiwa na raisi wetu wa

Kwa heshima kubwa kwa sekta ya mtindo nchini Tanzania, FAT hufanya uchambuzi na kupeleka mitindo katika ngazi ya juu kupitia njia inayofaa zaidi.  Kwa uimarishaji huu, shughuli zetu zinategemea nguzo tatu za usaidizi kamili kwa njia ya programu, kuimarisha mara kwa mara kupitia mwongozo na kupeana habari za mabadiliko ya vitu vipya au mwenendo katika sekta ya mitindo. Taasisi yetu inawigo mpana ulioambatana na shauku na jitihada endelevu katika kukuza sekta ya ubunifu na mitindo .

Kuhusu Fashion Association of Tanzania

Chama cha Wanamitindo Tanzania (FAT) ni shirika lisilo lisilotengeneza faida , lenye lengo la kundeleza maslahi ya sekta ya mitindo ya Tanzania kwa kuwaunganisha na kugawana ujuzi, uzoefu na rasilimali za sekta hiyo.

FAT yenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam, kimeundwa kufanya kazi  nchini na kuongoza sekta hii kupitia ushawishi wa kibunifu na kutumia njia sahihi za kuiweka Tanzania katika uchumi wa mitindo wa kimataifa.